Serikali Imeombwa Kutengeneza Utaratibu wa Kutoa Huduma ya afya Bure angalau mara Moja kwa mwaka kwa wananchi wake kupitia vituo vya afya vya serikali na Binafsi ili kufikia Makundi yasiyo na Uwezo wa Kumudu Gharama za Matibabu.
Wakizungumza mara Baada ya kupatiwa Matibabu ya afya Bure katika kituo cha afya cha Ololien Community Mkoani Arusha, baadhi ya wananchi walio fika kupata huduma hiyo wamesema vituo vya afya vya serikali na Binafsi vinatakiwa kutoa huduma hizi mara kwa mara ili kufikia makundi ambayo haya uwezo wa Kumudu Gharama za Matibabu ikiwemo watoto waishio Mazingira Magumu.
Dokta Robert Byemba ni Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Ololien Community ambapo amesema Kituo hicho cha afya kimeshirikiana na Halmashauri ya Arusha Kutoa huduma hiyo ya kutibu wakazi wa eneo hilo bure baada ya Kuona Uhitaji wa makundi ambayo yamekuwa yakishindwa kumudu gharama za vipimo na Dawa hali inayo sababisha kuugua na hata Kifo.
Kwa upande wake Afisa utawala wa Kituo hicho cha afya Filbert Jeremia amebainisha kuwa kwa mwaka 2022 wamefanikiwa kutoa huduma ya Afya Bure kwa wananchi mara tatu katika mikoa ya Arusha na Manyara huku wakiwa na Malengo ya kufika Mikoa mbalimbali hasa Vijijini.
Katika Tukio Hilo la Kutoa Huduma ya Afya kwa wananchi, Zaidi ya wakazi Elfu moja (1000) Kutoka eneo Hilo la Ololien Mkoani Arusha wamepatiwa Matibu ya Afya Bure kutoka Kituo cha afya cha Ololieni Community.
Kwa Mujibu wa shirika la afya Duniani Inaeelezwa kuwa Utoaji wa Huduma za fya Bure kwa wananchi Husaidia kufikia Jamii ya watu wasio jiweza kupata matibabu hasa ya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza.inasubiri kuridhiwa.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Dr. Robert Byemba
Huduma : Huduma za Afya Bure
Mahali : Arusha | Olorieni
Kanisa : Baptist
Contact : +255 754 67 56 82
No comments:
Post a Comment