Wananchi Wametakiwa kuibua Ukatili ambao umekuwa ukifanywa na Viongozi wa dini badala ya Kufumbia macho kwa kuamini kuwa ni kulibomoa kanisa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Muwezeshaji kutoka shirika lisilo la Kiserikali linajihusha na masuala ya Kijamii Fida International kupitia Mradi wa Cycle Social Support Yusto Swai amesema Ukatili ndani ya Kanisa umekuwa hautajwi licha ya Kuwa unafanyika kwa siri.
Emammnuel Tille ni Mkaguzi kutoka Jeshi la Polisi kata ya Ngarenanyuki amesema semiana hii ya Kuzuia Ukatili katika Jamii itawasaidia kupunguza Matukio ya Kihalifu kufuatia jamii ya Kimasai kuwa na Mila Pingamizi.
Mary Mbise ni afisa maendeleo kata ya Kingo’ri ambaye alifanikiwa kushiriki mafunzo ya jinsi ya Kuzuia ukatili ngazi ya Jamii amesema mafunzo haya yatamsaidi kufikisha elimu kwa Vikundi mbalimbali ikiwemo Vikoba shuleni na Vikundi vya Akinamama jinsi ya Kuripoti taarifa za Ukatili.
Makundi Yaliyo shiriki katika mafunzo haya ya Kuzuia ukatili ngazi ya Jamii ni Jeshi la Polisi kitengo cha Upelelezi wilayani Arusha, Maafisa maendeleo ya Jamii, Madiwani na watendaji wa kata.
Ripoti mpya iliyotolewa tarehe 18 Juni 2020 na Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kimataifa ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto imeonya kwamba nchi zimeshindwa kuzuia ukatili huo dhidi ya watoto na kutoa wito kwa nchi kuchukua hatua kuzuia athari kubwa zaidi.
Kwa Mujibu wa UNICEF Bilioni 1 ya watoto ni waathirika wa ukatili wa kimwili,kijinsia,kisaikolojia na kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment