Bahati Bukuku  ni muimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili nchini Tanzania ambaye amesimulia jinsi alivyolazimika kubeba maiti ya mtoto wake kwa daladala.
 
Bahati anasema alifiwa na mtoto wake baada ya mimba zake nyingi kuharibika, suala ambalo aliyekuwa mumewe, Daniel Basila alishindwa kulivumilia na kusababisha ndoa yake kuvunjika.
 
 Bahati anasema; “Baada ya kujifungua mtoto wangu alifariki dunia baada ya kulazwa hospitalini kwa muda, nilijaribu kumpigia simu aliyekuwa mume wangu, lakini hakupokea simu zangu.”
 
Bahati anasema madaktari walikuwa wakimhimiza kulipa bili kabla ya kumruhusu kuchukua maiti ya mtoto wake ambapo bili hiyo ilikuwa ni zaidi ya shilingi milioni moja.
 
 “Sikuwa na pesa za kulipa bili kwa hiyo nilimwambia daktari anipe maiti ya mtoto wangu au azike mwenyewe,”anasema Bahati.
 
Bahati anasema alipewa mwili wa mtoto wake, lakini hata hivyo alishindwa kuusafirisha kwa kukosa pesa za kukodi gari ikabidi atumie usafiri wa daladala kusafirisha maiti hiyo, tulimfunga mtoto na kushika kama mzima, hakuna mtu ambaye angeweza kugundua kirahisi.
 
Bahati anasema alifanya jitihada hizo akiwa mwenyewe huku aliyekuwa mume wake akiwa bize na mambo yake.
 
“Tukio hilo lilinifanya nijaribu kujiua ikiwemo kunywa sumu na kusababisha kuwachukia wanaume wote kwa wakati huo, nilisimamisha hata huduma yangu ya kuimba, nilijua ndiyo mwisho wangu, lakini namshukuru dada yangu, Jenipher Mgendi alinitia nguvu na kunishika mkono nikasimama tena na kupendwa na Watanzania mpaka leo nina furaha tena,” anamalizia Bahati.

BAHATI BUKUKU: NILIMWAMBIA DAKTARI ANIPE MAITI YA MWANANGU AU AZIKE MWENYEWE

No comments:

Post a Comment