Klabu ya Mtibwa Sugar itakuwa na kibarua kizito katika uwanja wa Azam Complex Chamazi siku ya Jumamosi pale itakapo shuka dimbani kuikabili Azam FC mchezo wa robo fainali wa kombe la Shirikisho majira ya saa 1: 00 usiku.
Mabingwa hao mara mbili wa ligi kuu soka Tanzania Bara kutoka mji kasoro bahari, watawakosa wachezaji wao wawili wanao cheza katika nafasi ya ulinzi ambao ni Issa Rashid “baba ubaya” na Salum Kupela Kanoni “mbavu kunesa” wakati wengine wakitarajiwa kuwemo ndani ya kikosi hicho.

Kocha mkuu, Zuberi Katwila ameelezea nafasi ya Mtibwa Sugar kuelekea kwenye mchezo huo wa robo fainali.

Kila timu iliyofika hapa katika robo fainali ya kombe hili ni nzuri hivyo tunajua tunaenda kupambana na timu nzuri ila tumejipanga kwa ajili ya kuwaletea furaha na heshima wana Mtibwa Sugar

Kikosi cha wana tamtam kinaendelea na maandalizi yake katika dimba la Manungu mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo huo wa Azam Sports Federation Cup.

Mtibwa Sugar kuwakosa wachezaji muhimu dhidi ya Azam FC

No comments:

Post a Comment