Mwanamume mmoja nchini Uingereza amesemekana kuwa na kesi “mbaya zaidi” duniani ya ugonjwa wa Kisonono.
Alikuwa na mpenzi mmoja nchini
Uingereza lakini alipata bakteria hiyo baada ya kujamiana na mwanamke
mmoja kutoka Kusini Mashariki mwa Asia.
Madaktari wa afya huko Uingereza
wamesema kwa mara ya kwanza kwamba maambukizi hayo hayawezi kutibika na
dawa aina za ‘antibiotics’
Maafisa hao sasa wanamtafuta
mpenzi yeyote wa mwanamume huyo, ambaye bado hajulikani, kama njia ya
kujaribu kuzuia usambazaji zaidi.
Mwanamume huyo alipatwa na mambukizi hayo mapema mwaka 2018.
Tiba halisi ya ugonjwa huo ni mchanganyiko wa dawa aina ya azithromycin na ceftriaxone lakini zimeshindwa kuutibu ugonjwa huo.
Dkt Gwenda Hughes, wa kituo cha
afya cha Uingereza amesema: ”Hii ni mara ya kwanza kwa kesi kama hiyo
kudhihirisha kiwango kikubwa cha kutosikia kwa dawa hizo mbili
zinazotumika sana za antibiotics.
Majadiliano na Shirika la Afya
Duniani(WHO) na kituo cha ulaya kinachodhibiti magonjwa wamekubaliana
kwamba kisa hicho ndicho cha kwanza kutokea duniani.
Kisonono ni ugonjwa gani?
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria kwa jina Neisseria gonorrhoeae.
Maambukizi hayo husambazwa na ukosefu wa kinga mtu anapofanya kitengo cha ngono.
Kwa wale walioambukizwa, mwanamume
mmoja kati ya10 na zaidi ya robo tatu ya wanawake na mashoga dalili za
ugonjwa huo hazibainiki kwa haraka.
Dalili za ugonjwa huo zinajumuisha;
- Ute mzito wa rangi ya jani au manjano kutoka katika sehemu za siri,
- Uchungu unapokojoa
- Uvujaji damu wakati mwengine.
Maambukizi hayo wasipotibiwa
yanaweza kusababisha mtu kukosa mtoto, kufura katika sehemu za siri na
unaweza kusambazwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto aliyetumboni.
Utafiti wa mwanamume huyo unabaini
kwamba ‘antibiotic’ ya mwisho inaweza kufanya kazi . Kwa hivi sasa
anapokea matibabu na madaktari watapata matokea baada ya mwezi mmoja
iwapo watafaulu.
Kwa hivi sasa hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa -hata mpenzi wake wa Uingereza amegunduliwa lakini uchunguzi bado unaendelea.
Dkt Hudhes aliongeza:
”Tunafuatilia kesi hii ili kuhakikisha kwamba maambukizi hayo yametibiwa
vilivyo na mapendekezo mengine na hatari za maambukizi kwa siku zijazo
kupunguzwaa.”
Dkt Olwen Williams, rais wa
muungano wa Uingereza wa maswala ya afya ya ngono na virusi vya HIV:
”Kutokea kwa maambukizi hao ambayo hayasikii dawa ya kisonono ni jambo
la kuzingatiwa na maendeleo makubwa.
”Tunawasiwasi kwamba shida hii inaweza kuongezeka kutokana na upungufu uliofanyiwa bajeti ya afya.
”La kusikitisha kabisa ni kwamba
kesi hii imeiwacha huduma ya afya ya ngono katika nafasi ”mbaya” huku
kliniki zikifungwa katika wakati mgumu zaidi.
Chanzo:BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment