Imeelezwa kuwa
wanakwaya 4 wamefariki na wengine
18 wamepote wakienda krismas mkoani kigoma baada ya Boti ya MV Pasaka
iliyowabeba katika kuwapelea shughuli za Ibada za kuelekea Krismasi kwa kugongana uso kwa uso na Boti .
Boti hiyo imegongana na boti nyingine iitwayo MV Atakalo
Mola na kuzama ziwa Tanganyika tukio ambalo limetokea majira ya Saa 9:15 siku
ya ijumaa katika kitongoji cha Lubengela wilaya ya uvinza Mkoani Kigoma.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Martini Otieno
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo
Aidha chanzo cha
ajali hiyo kwa mujibu wa Ofisa Mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu
SUMATRA mkoni Kigoma Amaniel Sekule amesema ni kwa sababu ya kiza kinene na
boti zilikuwa za Kienyeji.
No comments:
Post a Comment