Mwalimu
wa Shule ya Sekondari Kihenya, wilayani Kasulu mkoani Kigoma, ameuawa
kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi akiwa nyumbani
kwake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP James
Manyama, alisema tukio hilo limetokea Septemba 6, majira ya saa tatu
usiku, baada ya watu hao kuvamia nyumba ya mwalimu Fredrick Richard
(30), aliyekuwa akiishi na mke na watoto wawili.
Alisema
watu hao hawakuongea neno lolote baada ya kuingia ndani, walimpiga
risasi mwalimu huyo na kuondoka bila kuchukua kitu chochote.
Jeshi
hilo linamshikilia mtu mmoja akihusishwa na mauaji hayo baada ya polisi
kuokota kofia katika eneo la tukio iliyosaidia kumpata mtuhumiwa huyo
huku watuhumiwa wengine wakiendelea kutafutwa ili waunganishwe na
mwenzao.
Kamanda
alisema huenda tukio hilo ni la kulipa kisasi kwa kuwa wahalifu baada
ya kutekeleza mauaji hawakuiba, hivyo kuwataka wananchi kuacha
kujichukulia sheria mkononi.
No comments:
Post a Comment