Na Hekima Jonathani

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Innosmart Ndarishau  kutoka Himaya ya Mlima Meru ambaye Anazidi kufanya vizuri Katika Tasnia ya Nyimbo za injili hapa nyumbani Tanzania na baadhi ya Nchi jirani amesema anauwezo wa kutunga Nyimbo na kuziuza au kuzitoa Bure.

Amesema Tangu ameanza kuimba Miaka Miaka Mitatu iliyopita (3) amefanikiwa kutunga nyimbo zaidi ya Thelathini (30).

Innosmart ameyasema hayo wakati akitambulisha Wimbo wake mpya unaoitwa jina Nibebe kwenye  kipindi cha Topten kinachoruka kupitia 97.7 Habari Maalum fm.

Amesema kuwa talanta yake ya Uimbaji haikuanzia kwake  wala hakujifunza ukubwani kwani hata familia yake walikuwa ni waimbaji na wazazi wake pia walikua ni wanakwaya huko mkoani Tabora.

Amebainisha kuwa wimbo wake mpya wa nibebe alipata wakati mgumu katika kuchagua jina litakalo beba nyimbo lakini baada kumshirikisha MUNGU katika hilo hatimae akapata jina hilo la Nibebe.

"Kipindi nina tunga huu wimbo nilikuan nafikiria niuite salama au nibebe lakini kipindi natunga huu wimbo ilikua ni mwisho wa mwaka na wakati huohuo nilikua namuomba MUNGU anibebe kwa mwaka unaofuata katika huduma na maisha binafsi hivyo basi ndipo jina la nibebe liliponija."

Akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho kuhusiana na mapokeo ya nyimbo zake kwa watu amesema kuwa kumekua na shuhuda kwani amekua akipokea Mrejesho kutoka kwa watu Tofauti Tofauti wasikilizaji wa nyimbo zake kuwa wengi wao wamekuwa wakibarikiwa na nyimbo hizo jambo ambalo anarudisha utukufu kwa aliye juu.

Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa kuhusiana na huduma kuna kazi nyingi kwa mwaka huu zinakuja na kwa uwezo wa  MUNGU mwaka huu huduma itakua ni kwa viwango vingine hivyo basi kwa wale Wadau na wapenzi wa muziki wa injili wakae mkao wa kula.

Innosmart Ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili ana uwezo wa Kutunga nyimbo na Kumtungungia Mwimbaji Mwenzake mbali na Uimbaji ni mfanya Biashara wa Vipuli vya Magari mkoani Arusha.

CHANZO CHA HABARI

Jina : Innosmart

Huduma : Mwimabji wa Nyimbo za Injili

Mahali  : Arusha

Contact : +255757457376

KUTANA NA MWIMBAJI WA GOSPEL AMBAYE ANA UWEZO WA KUTUNGA NYIMBO ZA INJILI NA KUZIUZA AU KUZITOA BURE

1 comment: