Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa H. Aweso (Mb) ametengua uteuzi wa Meneja wa Maji Mkoa wa Dodoma, (RUWASA) Mhandisi Godfrey Kabula Mbabaye.
Waziri Aweso amechukua hatua hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Na. 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Aidha, Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba
kuunda timu ya Wataalam ya kufuatilia changamoto ya utekelezaji wa
Miradi ya Maji kwa Mkoani Dodoma na kutoa suluhisho la kumaliza
changamoto hizo mara moja.
Vilevile, ameelekeza timu hiyo ya Wataalam itakayoundwa na katibu Mkuu
ifanye tathimini ya utendaji kazi wa Mameneja wa Wilaya zote wa Maji
Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment