Kampeni ya Kamata wote Inayo fanywa na Mmamlaka ya Mapato Tatanzania TRA mkoa wa Arusha imefanikisha zoezi la Mshine EFDs 526 kununuliwa Huku Zaidi ya Kesi 76 zikifunguliwa kwa makosa ya Kushindwa kutoa na Kudai Risiti.
Hayo yamesemwa na Afisa msimamizi wa kodi TRA Mkoa wa Arusha Walter Mollel katika kipindi cha amka ungaze Kinacho Peperushwa Kila asubuhi Jumatatu hadi Ijuma Habari Maalum Media.
Akibainisha Muendelezo wa kampeni hiyo Kitaifa ya Kamata Wote Asiye toa na Kudai Risiti amesema tangu Imeanza Mkoa wa Arusha hati za makosa zilizotolewa ni 74.
“Kuna wale wateja ambao wao walishindwa kudai risiti zao za EFDs hao tuliwapata pia walikua wateja 18, wafanyabiashara ambao walishindwa kutoa risiti za EFD chini ya kiwango wao walikua 34, tulikua tuna wafanyabiashara ambao wao walishindwa kununua mashine ya EFD wakulima ni 5” Alisema Afisa Kodi TRA mkoa wa Arusha Walter Mollel.
Aidha amebainisha Kuwa kuna wafanyabiasha ambao walifikia vigezo vya kusajiliwa kwenye ongezeko la thamani lakini walikua bado hawajasajiliwa wao walikua Wawili (2).
“ Tuna wafanyabiashara ambao pia walifanya makosa vya stemp za vinywaji tulimpata 1,kuna wafanya biashara ambao walishindwa kutii kanunu mbali mbali wao walikua12,kwahio jumla walikua wafanyabiashara 74 hayo ndiyo makosa yaliyokamatwa kwa kipindi hiki kifupi”amesema mollel.
Aidha afisa huyo ameongeza kuwa kuna makosa mengine yaliyokwisha kukamwatwa kwa kipindi hiki kifupi ambacho wamefanya kampeni hio kwahio imekua na faida sana kwao maana wametambua niwapi panapofaa kurekebisha.
Pia amesema tangu waanze kufanya kampeni yao wamefanikiwa kununua mashine ya kufanyia kazi kwaajili ya wafanyabiashara mbali mbali ili waweze kujiajiri na kufanya kazi kuweza kujipatia kipato wenyewe sio kusubiri ajira ajipatie ajira binafsi.
“Tangu tumeaza kampeni hii ndani ya siku kumi mashine ya EFD mia tano yamenunuliwa kwahio na wafanyabiashara wapya mia tano ishirini na tano kwa mkoa huu wa Arusha wameweza kununua mashine ya EFD kitu ambacho ni ongezeko kubwa sana” Amesema mollel.
Hata hivyo Mollell Amehitimisha Kwa Kuwaomba wafanyabiashara kununua mashine za EFDs kwaajili ya biashara zao binafsi na Kujenga Taifa Kiuchumi.
No comments:
Post a Comment