Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kuongeza nguvu zaidi katika kusimamia utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini.

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo mara baada ya kuongoza zoezi la kufanya usafi katika soko kuu la wamachinga mjini Dodoma ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 05, 2023.

Kwa upande wake meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya kaskazini Lewisi Nzali amesema utunzaji wa mazingira sio wa NEMC peke yao bali jamii ishirikiane kwa pamoja katika utunzaji wa mazingira kwa kuwa ni wajibu wa kila mtu hasa kundi la vijana.

Vilevile ametoa wito kwa jamii kuwa na utamaduni wa kupanda miti kwenye maeneo yao pamoja na kuitunza ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo ambayo athari zake ni kubwa ikiwemo ukame.

Kwa upande Renalda Mlay ambaye ni mdau wa mazingira kutoka Jijini Arusha amesema jamii inapaswa kufahamu utunzaji wa mazingira kuwa ni wajibu wao hivyo wanapaswa kutunza mazingira.

Akiongea kwa niaba ya vijana wengine Edwini Silayo kutoka shirika la change mekar lililopo jijini Arusha linalohusika na maswala ya vijana amesema vijna ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo utunzaji wa mazingira ukinzia kwao utaleta matokeo chanya nchini Tanzania.

Hata hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira limeendelea kupewa kipaumbele hapa nchini ambapo leo ndio kilele cha siku ya mazingira duniani yakiongozwa na kauli mbiu ya Linda uchafuzi wa mazingira unaoto.

 CHANZO CHA HABARI

Jina : Lewis Nzali

Huduma :Makamo wa Rais / Meneja NEMC

Mahali  : Arusha

Mamlaka : NEMC

Contact : +255 762074043

NEMC: VIJANA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UKIANZIA KWAO UTALETA MATOKEO CHANYA

No comments:

Post a Comment