Mwimbaji na muandaaji wa tamasha la INUKA TENA CONCERT linalofanyika July 02, 2023 Chrispin Gabriel ametaja baadhi ya sababu zilizomfanya kutumia jina hilo kwenye tamasha ni kusimama kwa huduma yake kwa muda mrefu.
Akizungumza katika kipindi cha Gospel Climax cha Habari maalum Fm Chrispin aliulizwa swali hilo kwenye kipindi na kusema kuwa, zipo sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kusimama kwa huduma yake kwa muda na sasa kunaweza kuinuka upya tena.
"Kwa sababu binafsi kuna mahali nilitulia kidogo lakini nilitaka kusimama kufanya kazi kwa upya tena kufanya kazi ya Mungu hivyo jina likanijia na nikaamua kuita jina hilo"Alisema Chrispin.
Aliongeza KUWA, zipo sababu nyingi za kuita kina hilo ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo watu wanaopita kwenye nyakati ngumu kuwa wanaweza kuinuka tena na kusonga mbele.
Ikumbukwe kuwa Tamasha la INUKA TENA CONCERT litakalofanyika siku ya jumapili Juni 2/2023.kuanzia saa 8 mchana kwenye kanisa la Naivera church Apostolic Ungalimited Arusha.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Chrispin Gabriel
Huduma :Mwimbaji wa Nyimbo za Injili
Mahali : Arusha
Mamlaka : Huduma
Contact : +255 718546073
No comments:
Post a Comment