HUU ndiyo umafia hii ni baada ya mabosi wa Simba wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ wamefanikiwa kuinasa saini ya winga wa kulia wa kimataifa wa Niger, Victorien Adebayor muda mchache kabla ya kuivaa Taifa Stars juzi Jumapili.

Mabosi wa timu hiyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanaijenga upya timu yao kufuatia kufanya vibaya msimu uliopo kwa kushindwa kutwaa mataji.

Katika Ligi Kuu Bara wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Mabingwa Yanga wakati kwenye Kombe la FA wakiishia nusu fainali huku Ligi ya Mabingwa Afrika wakimaliza kwenye robo fainali.Kufanya vibaya huko kumepelekea mabosi wa timu hiyo kuanza kushusha vyuma mapema ikiwa tayari wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Onana Esomba kutoka Rayon Sport ya Rwanda kabla juzi kukamilisha usajili wa Abebayor ambaye alikuwa nchini na timu yake ya Taifa ya Niger.

Vigogo wa Simba walichokifanya kuweza kufanya mazungumzo na mshambuliaji ya kukubali kujiunga na timu hiyo ni baada ya kuvamia kambi ya Niger iliyokuwa katikati ya mitaa ya Jiji la Dar ambapo ilifikia timu hiyo kabla ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya AFCON.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza kuwa Simba wamekubaliana kila kitu na winga huyo juu ya kujiunga na timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa kwa mkataba wa miaka miwili huku Simba wakilazimika kuwafuata RS Berkane ili kukamilisha usajili huo.
“Viongozi walimfuata mchezaji katika hoteli ambayo amefikia na timu yake na wamefanikiwa kufanya mazungumzo, mchezaji mwenyewe amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili lakini amewaeleza namna ambayo alikosa nafasi kubwa ya kucheza kule Morocco.

“Lakini kwa sasa kilichobakia ni kwa viongozi wa Simba kwenda Berkane kumaliza nao ili kila jambo likae sawa na kuna uwezo wa mtu kutumwa kwenda Morocco wakati wowote.”

Lakini kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Gain’, alishaweka wazi juu ya suala la kuboresha benchi la ufundi la timu hiyo kwa kusema kuwa wanayajua makosa waliofanya msimu huu hivyo wamejipanga kufanya maboresho makubwa katika benchi la ufundi la timu hiyo ili kuweza kufanya vizuri msimu ujao.

UMAFIA WAFANYIKA DAR - ADEBAYOR ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA

No comments:

Post a Comment