Jeshi la Polisi Mkoa Arusha, linamshikia msichana Brandina Fred mkazi wa Kijiji cha IIkirev, Kata ya Olturoto wilayani Arumeru, kwa tuhuma za kumuuwa kwa kumchoma kisu mpangaji mwenzake, Erick Adam kutokana mchango wa sh 1000 za umeme.
Tukio hilo limetokea jana baada ya kutokea ugomvi baina ya wapangaji hao wawili ambapo inadaiwa marehemu Adam aligoma kulipia deni la umeme ambao kwa kawaida wapangaji huchangia.
Kamanda wa polisi mkoa Arusha, Justine Masejo akizungumza na Mwananchi leo, June 20, 2023, amesema tukio hilo lilitokea majina ya mchana wakati, Blandina akiwa na kisu akijiandaa na kupika.
No comments:
Post a Comment