Mamlaka
ya dawa na vifaa tiba Kanda ya Kaskazini imewataka wananchi kuacha
Tabia ya matumizi ya dawa kiholela bila kupata vipimo kutoka kwa
Wataalamu wa afya ili kupunguza Vifo vitokanavyo na usugu wa Vimelea vya
magonjwa dhidi ya Dawa.
Hayo Yamesemwa na Mkaguzi wa dawa na Vifaa tiba Kanda ya kaskazini (TMDA)
Dkt.Itikija Mwanga wakati akitoa elimu juu ya wiki ya Kidunia ya
Kuongeza uelewa kuhusu Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa
Habari Maalum Media.
Dkt.
Itikija amesema ili Kuepukana na vifo vitokanavyp na Usugu wa Vimelea
vya Magonjwa dhidi ya Dawa ni vema maeneo ya Makazi ya watu kuwa safi
na salama muda wote ili kuondoa Bakteria ambao wamekuwa chanzo cha
Vimelea Hivyo kutengeneza usugu.
Augustino Malamsha afisa Elimu kwa Umma kanda ya Kaskazini (TMDA)
ametoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya dawa kwani
kutumia dawa kiholela ni njia mojawapo inayoweza kupelekea usugu wa
vimelea dhidi ya dawa na Kuchangia vifo kwa Jamii.
Hata
hivyo Inaelezwa kuwa uchunguzi wa Tatizo la usugu wa vimelea vya
magonjwa dhidi ya dawa kwa mujibu wa WHO wamesema kwamba watu milioni
1.27 hufariki dunia kila mwaka kwa tatizo Usugu wa Vimelea vya Magonjwa
dhidi ya Dawa.
No comments:
Post a Comment