Mama Wajawazito wameshauriwa kuacha matumizi ya vileo pindi wanapojigundua wajawazito ili kumuepusha mtoto na madhara yatakayo msababishia matatizo ukubwani ikiwemo Ulemavu.
Akizungumza na kanzihabari Afisa Muuguzi kutoka hospitali ya Maternity Africa Ernest Benedict amesisitiza ni vema mama anapojigundua kuwa na ujazuzito kuepuka matumizi ya vilevi ili kulinda afya yake pamoja na ya mtoto tumboni.
Kwa upande mwingine amewaasa akina mama wajawazito kuepuka matumizi ya dawa kiholela bila ushauri wa daktari kwani yanaweza kuwa sumu kwa mtoto na kusababisha mimba kutoka,ulemavu kwa mtoto au hata kifo.
Nao baadhi ya akina mama wamesema wamekuwa na tabia ya kutumia dawa wanapokuwa wajawazito bila ushauri wa daktari na kukosa kujua madhara yake hivyo wameitaka serekali kupitia wizara ya afya kutoa elimu hiyo zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za wataalamu wa afya duniani zinaeleza kuwa kunywa viwango vya juu vya pombe wakati wa ujauzito inaweza kusababisha mimba kutoka, uzani wa chini kwa mtoto, matatizo ya akili kwa mtoto na kuchanganyikiwa.
No comments:
Post a Comment