Serikali Imetenga Zaidi ya Ekari 21000 Mkoani Dodoma kwaajili ya Mradi wa TOBOA NA KILIMO unao lenga kushirikisha Vijana Kupitia Kilimo ili kupunguza umasikini Kupitia Vijana.
Hayo Yamesemwa na Naibu waziri wa Kilimo Anthony Mavunde katika Maonyesho ya Kilimo yaliyo andaliwa na Taasisi ya Kilimo nchini Tanzania TARI Serian na Kufanyika katika Viwanja vya Taasisi hiyo Mkoani Arusha.
“Program Hii tunaianza katika Mkoa wa Dodoma kama eneo la Majaribio tunaanza katika wilaya ya Chamwino na wilaya ya Bahi tutaisafisha ardhi hiyo tutawapatia Vijana watalima na Tutawatafutia masoko” alisema Naibu Waziri
Hata Hivyo Naibu Waziri wa Kilimo Mh Anthony Mavunde ameweka bayana mkakati wa serikali katika kuwafanya Vijana wengi zaidi kushiriki katika sekta ya Kilimo ambapo amesema kwamba moja kati ya mkakati ni upatikanaji wa ardhi itayowekewa miundombinu rafiki ili kurahisisha shughuli ya kilimo.
No comments:
Post a Comment