Mwimbaji
na Mchungaji wa kanisa la Dreamers Center lenye Makao yake Daresalaam
Christina Shusho amefanikiwa kuchaguliwa kuwania Tuzo za EAEA kwa mara
Nyingine
Christina Shusho amechaguliwa katika Vipengele Vitatu
EAEA Peoples Choice, Best Female gospel Artist na EAEA Gospel Song Of
The Year ambapo Wimbo wa Shusha Nyavu Umetajwa.
Akizungumza
na Method Charles katika kipindi cha Top Ten ya Habari Maalum fm kinachorushwa katika
studio za habari Maalum Fm na Kuongozwa na Ngaramtoni Arusha Christina
shusho amesema kuwa lazima uwe una kitu unachokifanya alafu kile kitu
kinazungumze kwa Watu.
“lazima uwe na kitu kinachoonyesha kuwa una kitu watu hawawezi kukuona wewe bali ni kazi ndio inasema “amesema Christina shusho.
Aidha Shusho amesema anawaomba mashabiki wake wamuunge mkono ili waweze kufikia kusudi wanalotarajia kufikia kwa kumpigia kura.
“Nipende
kutoa shukrani zangu kwa mashabiki,marafiki na ndugu zangu wa kanda ya
kaskazini kwa ushirikiano wao walionionyesha na pia naomba waniunge
mkono kwa kunipigia kura ili tuweze kukamilisha lile kusudi “amesema
shusho.
Jinsi ya Kumpigia Kura Christina Shusho Unaingia katika
Mtandao wao wa www.eastafricaentawards.com Utachagua Vipengele alivyo
chaguliwa Kisha Utampigia Kura.
No comments:
Post a Comment