Kikao Cha halmashauri kuu ya Kanisa La The Free Pentecostal Church Of Tanzania (FPCT) Kilicho fanyika Njedengwa Dodoma Kimeadhimia kuwepo na Ushirikiano kati ya Kanisa la FPCT na Life Ministry.
Katika kuhakikisha mpango mkakati wa kanisa wa 2014/2024 wa kuleta mamilioni ya watu kwa Yesu kanisa limeamua kushirikiana na Life Ministry kuhakikisha wanawaleta watu kwa Yesu.
Mzonya amesema hivi karibuni kuna mpango watauzindua na wanaamini watashirikiana vizuri na FPCT katika kuwafikia wasio fikiwa na Injili.
Halmashauri kuu kupitia Askofu Mkuu FPCT Mch Stevie Mulenga amesema wao kama kanisa wanaona ni fursa nyingine kupitia Idara ya Injili na Umisheni kuhubiri kupitia njia wanazotumia life Ministry ikiwa ni pamoja na uonyeshaji wa sinema za Yesu katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment