Hayo yamebainishwa na Mchungaji Liberty Shirima katika Ibada ya Jumapili iliyo fanyika katika Kanisa la Yerusalemu Mpya Lililopo Kijenge Mkoani Arusha.
Mchungaji Shirima amesema kuwa Mkristo anapo Pitia Changamoto Humuabudu Mungu zaidi Ukilinganisha na Pale anapo kuwa hana Changamoto katika Maisha yake ya kilasiku.
Aidha amesema kuwa Mtu anapo kuwa na Madhaifu hujikita katika kumtafuta Mungu kwa Sehemu Kubwa ili kupata ufumbuzi wa madhaifu hayo.
Mchungaji Shirima amebainisha Madhaifu hayo ikiwa ni Pamoja na imani haba kwa baaadhi ya watu hali ambayo imekuwa ikiwasogeza zaidi na Mungu ili kuweza Kumjua Zaidi.
“Amesema Watu wakipokea vitu wanatakiwa kuviombea na kushukuru kwa Mungu kisha kuvitumia”Alisema Mchungaji Shirima,
Ametanabaisha kuwa Madhaifu mengine ni pamoja na magonjwa hali ambayo imekuwa ikimfanya Mkristo kuweza kuomba zaidi ili kuweza kuushinda mwili na kufanya kuwa karibu zaidi na Mungu.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Pastor Liberty Shirima
Huduma : Mchungaji Kiongozi
Mahali : Arusha
Kanisa : Yerusalemu Mpya
Contact : +255756364561
No comments:
Post a Comment