Waziri wa maji Jumaa Aweso amefanya makabidhiano ya kituo cha utafiti wa Ubora wa Maji Ngurdoto Kilichopo Mkoani Arusha kwa chuo cha maji Taifa ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama katika wilaya ya Arumeru.
Akikabidhi Kituo Hicho Mapema Wiki hii waziri Jumaa Aweso amesisitiza kuwa Upatikanaji wa maji Yaliyo Bora na Salama Yasiyo na Floride unatakiwa kufanyika kwa haraka Huku akitoka Kiasi cha Shilingi Millioni 100 ili kutatua Changamoto zilizopo katika Kituo Hicho ili wanachi waweze kunufaika na ubora wa maji safi na Salama Kupitia Kituo Hicho cha Utafiti
“Nataka mradi huu msisema mpaka bajeti ijayo, nawapa milioni mia moja muanze dizaini mapema na mradi ukamilike haraka , bunge la bajeti likikamilika na nyie mradi huu uwe umekamilika na huu mradi mhe: Mbuge nitakuja kuuzindua mwenyewe”Amesema Waziri Jumaa Aweso.
Hata hivyo Mbunge wa wilaya ya Arumeru Mashariki Dkt. John Pallangyo mempongeza Waziri wa maji kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na maji safi hasa kuweza kumtua mama ndoo kichwani.
“Tunaona unavyohangaika ili kuhakikisha tunamtua mama ndoo kichwani kazi unaifanya vizuri mno lakini pia nikupongeze kwa kuaminiwa ukaweza kuitumia nafasi yako vizuri kama Waziri wa maji hii ni kwa sababu ya uchapaji kazi wako ulivyo mahiri na tunakuombea kwa Mungu uendelee kuwa na afya njema na uzidi kutenda kazi hivyo hivyo”Alisema Mbunge Dkt John Pallangyo.
Mkemia Mkuu wa Kituo hicho cha Utafiti Masumboko Msongo amesema Kituo hicho kinatumia Teknolojia ya Chenga za Mkaa inayotokana na Mifupa ya Ng'ombe na Kuondoa Madini ya Floride.
Vile vile Mkuu wa Chuo Cha Maji Dkt. Adam Karia amesema kuwa wamekipokea kituo hicho kwa moyo na wanaahidi kukiendeleza vizuri kwa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa wanakifikisha mahali pazuri na panapostahili.
“Nakuahidi kuwa tumekipokea kituo hiki vizuri na mimi ni mmoja wapo wa watu waliokua wakifanya ziara hapa na kuona kazi ambazo zilikua zikiendea, nimefurahishwa na jitihada zinazofanywa na chuo hiki nakuahidi nitakifanya chuo hiki kiendelee katika hatua ambayo unaitamani”Amesema Mkuu wa kituo Dkt. Adam Karia.
Kituo cha utafiti wa Ubora wa Maji Ngurdoto Kitawanufaisha Wananchi wa wilaya hiyo wapatao laki 726,000 huku Vijiji 157 Vilivyo Wilayani Humo Vikitarajia Kunufaika na Mradi Huo.
No comments:
Post a Comment