Na Hekima Jonathani
Wakristo Wametakiwa Kusimama Imara Katika Misingi Ya Kristo ili Adui Muovu Shetani Asipate Nafasi Ya Kuwanyanyasa Katika Maisha Yao Ya Kila Siku.
Hayo Yamesemwa na Mwinjilisti Dkt. Pendael Sikawa Katika Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Kanisa la Fpct Nkwaranga Meru.
Akitolea Mfano Wa Daudi Na Wafilisti Katika Kitabu Cha Samweli Wa Kwanza Amesema Kuwa Daudi Hakurudi Nyuma Licha Ya Kutoaminiwa Na Wanadamu Alijua MUNGU Atamsaidia Kupambana na Goliath.
Mwinjilisti Dkt. Sikawa Alisema Kwa Kuangalia Akili Na Mawazo Ya Kibinadamu Unaweza Ukajiona Unaweza Peke Yako, Pengine Ni Kutokana Na Cheo Ulichonacho Au Nafasi Uliyonayo Sehemu Fulani Lakini Kumbe Shetani Anatumia Nafasi Hiyo Uliyonayo Kukupiga Sehemu Mbalimbali Katika Maisha Pengine Ni Katika Afya Au Mahusiano Yako Ya Ndoa.
“Kuna Watu Ambao Wanaweza Wakakudharau Kutokana Na Mazingira Uliyonayo Ni Haki Yao Kukudharau Kwa Sababu Hawajakuumba Na Hawajui Agano Uliloingia Na MUNGU Imefika Mahali Baadhi Ya Wakristo Wamejidharau Wenyewe Na Hii Kutokana Na Badhi Ya Mapito Wanayopitia Katika Maisha.”Alisema Mwinjilisiti Dkt. Sikawa.
Aidha Amesema Washirika hawana Budi Kuondoa Shaka Kwani Kila Jambo huwa lina wakati wake Wanatakiwa Kuomba, Kusubiri na Kuamini Kuwa Mungu anaweza Kubadili hali iliopo sasa na Kuwa katika Hali ya Tofauti.
Amebainisha Kuwa Mtu wa Mungu hatakiwa Kuacha Kuomba kwani aina ya Maombi Ya Kukomboa Yana Nguvu ya Kuuufanya Mwaka kuwa Wa Urejesho Kwa Kila Aaminiye.
Hata Hivyo Baadhi Ya Waumini Katika Kanisa Hilo Ambao Waliweza Kushiriki Katika Ibada Hiyo Walionyesha kuguswa Na Kubadilika kupitia Neno La Siku Hiyo Na Wanaamini Yale Ambayo Yalikua Yamefungwa Kwao Yanakwenda Kufunguliwa kupitia Maombi na Neno ambalo walijifunza.
CHANZO CHA HABARI
Jina : Dkt. Pendael Sikawa
Huduma : Mwinjilisti
Mahali : Kanisa la FPCT Nkwaranga
Contact: +255787074985
No comments:
Post a Comment