ARUSHA

Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Arusha Mhashamu Baba Askofu Izack Amani amewataka wakristo kutambua Nguvu ya Mungu iliyopo katika msalaba ambao ndiyo utambulisho na ishara ya wokovu kwa kila aaminiye.

Akihubiri katika ibada maalum ya ijumaa kuu iliyofanywa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Arusha,Askofu Izack amesema kuwa msalaba ni alama ya wokovu kwa wakristo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddy Kimanta katika ibada hiyo amesema kuwa atasimama imara kuhakikisha ushirikiano wa umoja wa makanisa hayo unakuwa bora na imara.

Aidha Kimanta amekemea tabia ya watu wanaotumia mitandao ya jamii kupotosha umma huku akisema kuwa nchi inaongozwa kwa mifumo nasiyo kwa mitandao.

Sambamba na hayo Mwenyekiti wa Umoja huo Dkt.Stanley Hotay amewataka wakristo kumuomba Mungu awasaidie katika kipindi hiki ikiwa ni pamoja na kutulia,kujiheshimu na kuhudhuria katika nyumba za ibada.

 Hata Hivyo awali Akimkaribisha mgeni rasmi katika ibada hiyo Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini kati Askofu Dkt.Solomon Massangwa ameeleza kuwa ni vema wazazi na walezi wakawafundisha watoto wao mausia mazuri ili taifa liweze kuwa salama.

ASKOFU IZACK AMANI : MSALABA NI UTAMBULISHO KWA KILA AAMINIYE

No comments:

Post a Comment