Daktari mmoja nchini Nigeria amesisimua wengi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuandaa sherehe kwa sababu ya kupata talaka kutoka kwa mume wake. 

Wengi wanapoingia kwenye ndoa hasa zinazofungwa kidini au katika afisi za serikali hula kiapo cha kusema kwamba watakuwa pamoja kwenye shida na raha hadi kifo kiwatenganishe. 

Ndoa kama hizo zinapovunjika, wahusika mara nyingi huwa hawataki ijulikane kwani huchukuliwa kuwa jambo la aibu. 

Lakini mwanadada kwa jina Ikea Bello ambaye ni daktari, ameonyesha kwamba talaka inaweza kuwa kitu cha kufurahikia. 

Alichapisha picha na video za tukio hilo lake ambapo rangi ya mavazi ilikuwa nyekundu na kama vile arusi, alibadili mavazi mara kadhaa, akisema mojawapo ya mavazi ni mtindo aliona kwa muigizaji maarufu wa Nigeria Tonto Dike. 

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na marafiki wa karibu na wote wanaomuunga mkono. Ingawaje hakutoa taarifa ya moja kwa moja kuhusu talaka yake aliandika maneno ambayo yaliashiria kwamba mume wake alikuwa mbinafsi mno ambaye alitaka aangaziwe zaidi kwenye uhusiano wao. 

Ikea aliashiria pia kwamba alikuwa amejitoa kwenye uhusiano ambao labda siku za usoni ungemsababishia msongo wa mawazo. 

Sherehe hiyo ya talaka pia ilikuwa na keki ya rangi ya dhahabu na zambarau yenye maneno “I Do, I Did, Am Done. Divorced At Last”. 

Mrembo huyo hujihusisha na maswala ya ushauri wa maisha.

DAKTARI ASHEREKEAA TALAKA

No comments:

Post a Comment