Mwanza.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza, amesema nchi inahitaji katiba mpya itakayogawanya madaraka na kutengeneza uhuru na uimara wa taasisi kufikia ufanisi na maendeleo endelevu ya Taifa.
Amesema wakati katiba ikiwa muhimu, haiwezekani kutenganisha uhuru na maendeleo au kuwafanya wananchi kuchagua kimoja kati ya vitu hivyo kwa kuwa vinakwenda sambamba.
Akizungumza na Vyombo vya habari katika mahojiano maalumu ofisini kwake mjini Karagwe katikati ya wiki hii, Dk Bagonza alisema katiba ya sasa imerundika madaraka na mamlaka yote kwa Rais, ambaye licha ya kuwa na washauri, halazimiki kufuata ushauri wao pale anapoona inafaa.
No comments:
Post a Comment