Na Method Charles
Mkurugenzi wa hospital ya Selian Ngaramtoni mkoani Arusha Dr Amon Israel Martin amesema kuwa ujenzi wa wodi ya wagonjwa katika hospitali hiyo umekamilika kwa asiliamia mia moja huku wodi hiyo ikiwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wagonjwa 50.
Ameyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha maisha ni changamoto katika studio za redio Habari Maalum alipokuwa akizungumza kuhusiana na huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo ya Seliani Ngaramtoni.
Akielezea ubora wa wodi hizo na wodi zingine amesema kuwa wodi hizo zina kifaa maalum ambacho anakitumia mgonjwa kumjulisha muuguzi kama anatatizo lolote pale atakapo muhitaji katika Kitanda chake.
Dr Amon amesema kuwa wameweka mfumo maalum unaowasaidia wagonjwa kutibiwa haraka zaidi wanapoenda kutafuta huduma za matibabu ukilinganisha na hospitali zingine.
Aidha ameongeza kuwa licha ya kuwa kumekuwepo na uhaba wa upatikanaji wa dawa kwa wagonjwa wanapoenda kutafuta matibabu wao wamejitahidi kuhakikisha kwamba dawa zinapatika kwa wakati pale ambapo mgonjwa anahitajika kupata dawa hizo.
Hatahivyo amesema kufuatia kuwepo kwa uhaba wa manesi katika baadhi ya hospitali wao wamejitahidi kuhakikisha wanakuwepo na wauguzi wakautosha katika hospitali hiyo wanaoweza kuwahudumia wagonjwa wengi kwa muda mchache.
Chanzo cha Habari
Mkurugenzi Selian Ngaramtoni : Dkt. Amon Israel Marti
Contact : +255754744232
Mahali : Arusha Ngaramtoni
No comments:
Post a Comment