Chama cha wanahabari Tanzania TAMWA chini ya Mradi wa Wanawake wanaweza unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalo hudumia wanawake UN Woman imezindua mafunzo kwa wanahabari 50 wa Redio za Kijamii kutoka katika mikoa 17 ya Tanzania. 
 
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddy Kimanta katika ukumbi wa Palace Hotel mkoani Humo ambaye alikuwa Mgeni Rasmi.
 
Mafunzo hayo kwa wanahabari yanalenga kuwajengea uwezo wa namana ya kuripoti kuhusu ushiriki wa wanawake katika uongozi na kuondoa Mifumo kandamizi inachochea ukatili wa wanawake na kukosesha fursa mbalimbali.
 
Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Kimanta amesema ni vema wanahabari kuongeza uwezo katika elimu ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa waledi na ubora.
 
Jukumu la Tamwa katika Mradi huu ni kushirikiana na Vombo ya Habari hasa redio za kijamii kuongeza uelewa kwa umma kuhusu umuhimu wa kuwezesha wanawake kutambuliwa na jamii kuwa viongozi halali.
 
Dokta Rose Reuben ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA amesema baada a Mafunzo hayo wanahabari hawa wa Redio za Kijamii wataanda vipindi vya Redio vitakavyo elimisha na kutambulisha wanawake kuwa wanastahili kuwa viongozi halali.
 
Hata hivyo Kwa Upande wake Muwezeshaji katika Mfunzo hayo ya Wanahabari Dastan Kamanzi amesema katika Mafunzo hayo watawasaidia Wanahabari kuwa na uwezo Bora wa kubaini Changamotlo ambazo zinawakumba Wanawake na Kupaza sauti Kuhusu changamoto hizo.
 
Chanzo cha Habari
Tamwa
Mahali : Arusha Tanzania

WANAHABARI 50 WA REDIO ZA KIJAMII TANZANIA WAPEWA MAFUNZO JINSI YA KUANDIKA HABARI ZINAZO HUSU WANAWAKE

No comments:

Post a Comment