Muimbaji wa nyimbo za injili Lyidia Livingstone anatarajia kuwa na Tamasha kubwa la miaka kumi ya huduma ya nyimbo za injili utakao fanyika Mwishoni mwa juma hili siku ya Jumapili.
Akizungumza katika Kipindi cha Top Ten ya Habari Maalum fm 97.7 kipindi kinacho Sikika kuanzia Majira ya saa kumi na Moja jioni hadi saa Moja Jioni na Kuongozwa na Mtangazaji Mahili wa Kipindi hicho Method Charles
Lydia Amesema Tamasha hilo la Miaka 10 ya Huduma yake litafanyika katika kanisa la Victory faith Mkoani Arusha Muda itakuwa kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni tamasha hilo litaambatana na uzinduzi wa Album itwayo Chineke.
Amesema sehemu ya pesa itakayo patikana ataitoa kwa wanawake kama mtaji kwaajili ya wanawake wanao ishi katika mazingira magumu kama mtaji wa kujikwamua kimaisha.
Ameongezea kuwa msaada huo atakao utoa kwa wanawake utakuwa ni katika mfumo wa muendelezo ikiwa ni Pamoja na kuwapa elimu ya kuserve pesa ambayo itawasaidia kuendeleza biashara zao.
Tamasha hilo litafanyika katika kanisa la Victory Faith lililopo Kijenge Mwanama jijini Arusha siku ya jumapili tarehe 18 mwezi wa kumi kwanzia saa nane kamili machana mpaka saa kumina mbili jioni.
Hata hivyo Lydia ameongeza kuwa uwepo wa wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili kama vile John Lisu ambae atakuwepo kwanzia kwenye ibada na baadae katika tamasha hilo la kihistoria Pamoja na hayo Lidya atashirikiana na waimbaji wa kanisahilo katika kumwimbia na kukumtukuza Mungu.
Chanzo cha Habari
Lydia Livingstone
Contact : +25756773895
No comments:
Post a Comment