Na Method Charles
Wachungaji wamehimizwa kuwekeza katika Idara ya vijana ndani ya kanisani na kutambua nafasi ya Kijana ili kuhimiza ukuaji wa Kanisa, Kiuchumi na Kiroho.
Hayo yamesemwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la AICT Majengo Arusha Dkt. Joseph Mayala katika kilele cha Siku ya Vijana kitaifa katika kanisa la AICT Tanzania.
Dkt. Mayala amesema ili kukuza Kanisa ni vema Wachungaji kuwekeza kwa vijana kwani vijana ni udongo laini na ni rahisi kupanda neno jema na likaota na kuleta matokeo chanya.
Akibainisha kuhusu sababu ambazo zimefanya idara ya vijana ifanikiwe na kuwa lulu ndani ya Kanisa hilo la AICT Majengo Arusha na Kufanikiwa kuanza kununua gari kwa ajili ya matumizi ya Kanisa amesema ni maombi na kufanya semina za mara kwa mara zinazowafanya vijana wajitambue na kubuni miradi mbalimbli za Maendeleo.
“Nimekuwa nikiomba na kufanya Semina mbalimbali za kuwajenga vijana ndani ya Kanisa ili hali ambayo inaonyesha matunda hayo ikiwemo mikakati ya kununua gari na hata kubuni Miradi mbalimbali yenye Mantiki kwa kanisa” Alisema Dkt. Mayala ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Compassion Tanzania.
Amesema Mstakabali wa Kanisa lolote lile nchini ni Wachungaji kutambua kundi la Vijana na hata kutambua madhaifu waliyo nayo kwa minajili ya kurekebisha na kuwalea ili kukuza Kanisa la leo.
Makula Monde Katibu wa Idara ya Vijana Kanisa la AICT Majengo Arusha amesema Idara hiyo inaratibu Mpango wa Kununua gari la Kanisa kwa sababu Kanisa bado halina gari kwa ajili ya kufanya Uinjilisti na kutembelea Jumuiya mbalimbali kwa ajili ya kuzifuatilia hali hii iliyo wasukuma kufanya hivyo.
Mwenyekiti wa Vijana katika Kanisa hilo Abel Mhela amesema katika wiki la vijana walifanikiwa kuwatembelea wagonjwa ambao hawana ndugu Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na kufanikiwa kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo kutoa damu.
Hata hivyo Mhela alifanikiwa kuweka Majumuisho katika ya Kazi zote walizo fanya kwa wiki nzima Mambo hayo yalikuwa ya kijamii, Burudani, Kiroho na Maendeleo Idara ya Vijana na Kanisa ikiwemo kipaumbele cha Kununua Gari kwa kufuata Wigo na Dira ya Kanisa Kitaifa kwa mpango Mkakati wa kanisa 2019-2024 jinsi idara ya ija Pastoreti a Majengo wanavyo Tekeleza
Chanzo cha Habari
Idara ya Vijana AICT Majengo Arusha
Contact : +255759468845
Mahali : Arusha Majengo
No comments:
Post a Comment