Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mohamed Maje kuanzia leo kwa kilichoelezwa kushindwa kutimiza majukumu yake.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tamisemi Mussa Iyombe inasema Maje
amesababishia hasara serikali ikiwamo kushindwa hata kukusanya mapato
ya serikali.
"Hata makusanyo ya mwaka huu hatujui anapeleka wapi hadi leo amekusanya
asilimia 24 tu katika halmashari ya Kongwa na Mpwapwa licha ya kuwa na
vyanzo vingi vya mapato.
Iyombe amesema Mkurugenzi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment