Kijana aliyetajwa kwa jina la Festa
Mtunga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 36 amekutwa
amekufa kwenye nyumba ya kulala wageni Chalinze mkoani Pwani.
Hadi sasa haijafahamika kijana huyo ni mkazi wa wapi.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Jonathan
Shana, amewaeleza waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kuwa,
tukio hilo lilitokea Machi 27 mwaka huu, saa 4:00 asubuhi huko Chalinze.
Shana amesema Festa alilala kwenye
nyumba hiyo lakini ilipofika asubuhi wahudumu walimgongea mlango bila ya
mafanikio na ndipo walipotoa taarifa polisi.
"Polisi ilibidi wavunje mlango na
kumkuta akiwa amelala peke yake kitandani, hakuwa na jeraha lolote
mwilini mwake baada ya uchunguzi na kuondoa mashaka juu ya kifo chake,"
amesema.
Ametoa wito kwa ndugu wa marehemu kujitokeza kuuchukua mwili huo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.
No comments:
Post a Comment