Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha (AUWSA) Imesema Mkataba Mpya Kwa Mteja Utanza Kutumika Hivi Karibuni baada ya Kuambatanisha maoni kutoka Kwa Wadau Mbalimbali wa Maji Jiji la Arusha.
Hayo Yamesemwa na Afisa Mahusiano Msaidizi wa Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha (AUWSA) Bi-Anny Mshana Katika Kipindi cha Amka Uangaze kinacho sikika Asubuhi Habari Maalum Fm.
Mshana amesema ili kupata Mkataba ambao utakuwa na Mmanufaa kwa pande zote mbili yaani Mteja na Mamlaka ya Maji walifanikiwa kufanya mkutano na Kukusanya Maoni ya wateja na wadau wakiwemo EWURA ili kutoa huduma kwa Usahihi.
“Sisi sote tunajua kuwa maji ni kitu muhimu sana kwa afya, kiuchumi majumbani hivyo basi Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha Itazingatia Mahitaji Yao” Amesema Anny Mshana afisa Mahusiano msaidizi Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha (AUWSA).
Aidha amesema kuwa wanafuata maagizo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya maji na kuambatanisha maoni ya wadau ili mkataba huo Uanze kutumika na kuleta Tija Kwa watumiaji wa Maji.
“Tunafuata sharia yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya maji lakini pia tuna Mamlaka Ya udhibiti wa maji ambao ni EWURA wao wanaangalia namna tunavyoendesha huduma yetu” Amesema Mshana.
Amesema kuwa huduma hiyo inamsaidia mteja kuelewa wajibu wa mamlaka kwa Mteja na wajibu wa Mteja kwa mamlaka.
”mkataba wa huduma kwa mteja unatoa muongozo sahihi kuisaidia mamlaka kushiriki kikamilifu katika majukumu yote tunayotakiwa kufanya kama mamlaka “Amesema Anny Mshana.
Vile vile amesema wanaendelea kufanyia kazi maoni ambayo yametolewa na wananchi ili mkataba huo uaze kutumika Hivi Kariubuni.
”Maoni yale yanafanyiwa kazi ili mkataba huo uaze kutumika kwa wananchi”
Ameongezea kusema mkataba huo hauna Muda mrefu utaaza kuwafikia wateja hivi karibuni na wananchi na watafikiwa huduma kwa karibu Zaidi.
Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha imeanzisha Mkataba Mpya kwa Mteja ili Kumsaidia Mtumiaji wa Maji kufahamu Wajibu wake kwa Mamlaka hiyo ili kusaidia Mmamlaka Kutoa Huduma Kwa Ubora.
No comments:
Post a Comment