Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgololo Kata ya Makungu pamoja na Shule ya Msingi Lugema Wilayani Mufindi kwa takribani wiki tatu wamekumbwa na tatizo la kuanguka, kutetemeka miguu (mwili), huku matukio hayo yakihusishwa na imani za kishirikina.

Hali hiyo imezua taharuki kwa wananchi wa Kata ya Makungu na kutaka kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali ikiwemo kuitwa kwa ‘lamba lamba’ jina ambalo limekuwa kubwa katika kata hiyo mpaka sasa likiwa na maana (Mganga wa kienyiji).

Aidha, baada ya siku chache kupita hatua hiyo ya kufikishwa kwa mtaalamu iligonga mwamba kutokana na msuguano kwa wakazi wa Kata ya Makungu huku wengi wao wakidai kuto amini ushirikina na kutaka kufanyika maombi ili kudhibiti tatizo hilo.

Hata hivyo, kiongozi wa kiroho kutoka Kanisa Katoliki Wilayani Mufindi Padre Shija amefika Shule ya Sekondari Mgololo na kuanza kutoa maji ya baraka hali iliyowasababisha wakazi wa kata hiyo kununua maji ili yabarikiwe kwa ajili ya kuwanyunyizia wanafunzi hao.

Wanafunzi wadondoka dondoka na kutetemeka shuleni

No comments:

Post a Comment