Meneja wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone anajipanga kufanya
usajili wa kushangaza kwa kumchukua mshambuliaji wa Leicester City,
Jamie Vardy.
Habari kutoka katika gazeti la Mirror la nchini Uingereza zinasema
Vardy mwenye umri wa miaka 31 anakadiriwa kuwa na thamani ya kiasi cha
paundi milioni 16 lakini Atletico Madrid wanapanga kutoa kiasi cha
paundi milioni 20 kiasi ambacho kitawashawishi Leicester kufanya
biashara hiyo.
Simeone anaamini Vardy atakuwa chaguo sahihi kurithi nafasi ya Antoine Griezmann ambaye anahusishwa na kutimkia Barcelona.
Atletico Madrid watalazimika kununua mshambuliaji mwingine atakaye
saidiana na Diego Costa ikizingatiwa kuwa Fernando Torres naye
anahusishwa na kutaka kuondoka katika klabu hiyo.
Simeone alivutiwa na kiwango cha Jemie Vardy katika ligi ya mabigwa
wa Ulaya msimu uliopita na sasa anataka mshambuliaji huyo atue katika
dimba la Wanda Metropolitano.
No comments:
Post a Comment