Mwalimu wa kike wa shule moja ya Sekondani katika eneo la Seme
nchini Kenya anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya
mapenzi ya jinsia moja na wanafunzi wa kike.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Kisumu, John Kamau amesema kuwa mwalimu
huyo anashikiliwa kutokana na mashtaka yaliyofunguliwa katika kituo cha
polisi na wanafunzi wanne wa kike wanaodai aliwafanyia vitendo hivyo.
Wanafunzi hao walioandika maelezo katika kituo cha polisi, wamedai
kuwa mwalimu huyo amekuwa wakiwaita nyumbani kwake katika eneo la
Kombewa na kuwafanyia vitendo hivyo.
Kufuatia malalamiko hayo, wanafunzi wa shule za bweni na wale wa
shule za kutwa waliandamana wakitaka hatua kali zichukuliwe na mamlaka
husika dhidi ya mwalimu huyo.
Jeshi la polisi linaendelea kumhoji mwalimu huyo na mashtaka rasmi
dhidi yake yatawasilishwa mahakamani, kwa mujibu wa jeshi hilo.
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na katiba ya Kenya, kama ilivyo kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment