Kocha wa klabu ya Newcastle United, Rafa Benitez ameekataa kukanusha
taarifa juu ya kutaka kumsajili Fernando Torres kutoka katika klabu ya
Atletico Madrid.
Akiongea na gazeti la michezo la ‘MARCA’ la Hispania, Benitez amesema
hajui kitu anachofikiria Torres kwa sasa lakini anadhani anawaza kwenda
sehemu nyingine japo itakuwa vigumu kutua Newcastle.
”Inafaa, lakini sidhani kama itakuwa rahisi”, alisema Benitez
alipoulizwa kama angependa kumsajili Torres. Kocha huyo ameongeza kuwa
wakati Torres akiwa Liverpool alikuwa bora zaidi na walipoungana katika
klabu ya Chelsea aliwasaidia kushinda kombe la Europa league japo hakuwa
na wakati mzuri katika klabu hiyo.
Akicheza chini ya kocha Rafa Benitez ndani ya klabu ya Liverpool Torres
alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 72 katika michezo 116 aliyoichezea
klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Liverpoool mwaka
2007 akitokea Atletico madrid kabla ya kurejea tena katika klabu hiyo
mwaka 2015 na tayari ameweka wazi kwamba huu ndio msimu wake wa mwisho
katika klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment