Askari polisi E. 1156 William Marwa
amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Tarime,
akikabiliwa na shtaka la mauaji ya Saguta Chacha ambaye ni mdogo wa
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.
Mshtakiwa huyo amesomewa kesi ya mauaji namba, PI 76/2018 mbele ya Hakimu A.R. Kahimba leo Aprili 30.
Askari huyo anayedaiwa kutenda kosa hilo
Aprili 27 hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka
ya kusikiliza shauri hilo.
No comments:
Post a Comment