Maaskofu watatu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) ‘wametengwa’ na kanisa hilo kwa tuhuma za
usaliti unaohusishwa na masuala ya kisiasa.
Mbali ya Askofu wa Dayosisi ya Mashariki
na Pwani, Dk Alex Malasusa aliyeripotiwa jana na vyombo vya habari
kwamba ametengwa, wengine ni Dk Solomon Massangwa wa Dayosisi ya
Kaskazini Kati na Dk Lucas Mbedule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki.
Hatua ya kuwatenga maaskofu hao
ilifikiwa katika mkutano wa Baraza la Maaskofu wa KKKT uliofanyika
Aprili 24 na 25 jijini Arusha kujadili masuala mbalimbali ikiwamo
kufanya tathmini ya waraka wake wa Sikukuu ya Pasaka lililoutoa Machi
24.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Baraza
hilo zinasema kwamba pia limewapa maaskofu hao watatu muda wa hadi
Septemba kuandika barua kueleza kama wanaukubali au kuukataa waraka huo
ambao limesema walishiriki kuuandaa na ikiwa hawatafanya hivyo hatua
zaidi dhidi yao zitachukuliwa.
No comments:
Post a Comment