Watu saba wakiwamo waganga wawili wa
jadi, wanashikiliwa na polisi wilayani Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma
za kupiga ramli na kusababisha familia tatu kukosa makazi baada ya
nyumba zao kuteketezwa kwa tuhuma za kishirikina.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa amewataja waganga hao kuwa ni Chemani Ndishiwa (79) na Nzali Mayunga (40).
Wengine waliokamatwa ni Masanja Seni
(65), Kasura Msomi (31), Michael James (19), Dotto Lukelesha (41) na
Samwel Jonas (18) wote wakazi wa kijiji cha Mwakwangu.
Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea
juzi Aprili 28, 2018 saa tano usiku katika kijiji hicho baadhi ya
wananchi walikwenda kwa waganga hao wawili kupiga ramli na kuambiwa
kijijini wapo baadhi ya familia ni wachawi.
Amesema baada ya kuelezwa hivyo, baadhi
wa wananchi waliamua kukodi vijana kwa kuwalipa fedha na hakuweza kutaja
kiwango waliokwenda kwenye nyumba ya Luli Lukeresha na kuichoma.
“Baada ya kufanya unyama huo, vijana hao
walikwenda tena katika miji mingine ambayo waliichoma na kutoweka
ingawa wananchi walitoa taarifa polisi Igunga,” amesema.
No comments:
Post a Comment