Mfanyakazi
'House Girl' mmoja wa ndani amemuua mwajiri wake Elizabeth Achieng
pamoja na kichanga chake chenye miezi mitatu huko Kisumu nchini Kenya.
Imedaiwa
kuwa mfanyakazi huyo alianza kwa kumpiga mtoto mpaka akamuua kisha
akamfuata mama yake na kumchoma kisu mara kadhaa na kisha kumchoma na
kitu kinachodhaniwa kuwa ni pasi ya umeme au tindikali.
Kwa sasa jeshi la Polisi Kisumu linamtafuta mfanyakazi huyo ambaye ametokomea sehemu isiyojulikana.
Taarifa zinasema kuwa katika tukio hilo mfanyakazi huyo hakumgusa binamu wa marehemu aliyekuwepo eneo la tukio.
Aidha
inasemekana kuwa mfanyakazi huyo alikuwa anaendana kiumri na mwajiri
wake kitu kilichokuwa rahisi kwa yeye kutekeleza tukio hilo.
No comments:
Post a Comment