Imeelezwa kuwa changamoto ya Upatikanaji wa Maji mkoani Arusha Itapungua Zaidi endapo Mvua zitaanza Kunyesha za Kutosha na Marekebisho ambayo yamekuwa yakifanywa na Mamlaka ya Maji Yatakamilika.
Akizungumza na Habari Maalum Fm Mkuu wa Mawasiliano na uhusiano na Umma kutoka katika Mamlaka ya maji mkoani Arusha AUWSA Masudi Katiba amesemaMamalaka inaendelea na marekebisho ya Kufufua Mabomba ya zamani ili Kuletea Ufumbuzi wa Maji katika baadhi ya Maeneo ya Jiji la Arusha.
Katiba amesema tatizo la upungufu wa maji ni kutokana na uhaba wa mvua katika Msimu ulio pita kufutia mabwawa mengi kutegemea mvua hivyo maji mengi Mamlaka Inategemea mvua ili kuongeza upatikanaji wa maji katika vyanzo vya Mito.
Amesema kuwa Visima havija athiriki na tabia ya nchi Kwani vimekuwa vikitumia umeme.
Masudi katiba amewasihi wananchi kwa kipindi hiki cha uhaba wa maji pindi yanapo toka wajitahidi na kuhakikisha kuwa wanachota maji ya Kutosha na kutumia kwa Matumizi Muhimu.
Moja ya Wananchi mkoani Arusha amesema Tatizo la limekuwa likitatuliwa Zaidi maeneo ya Mijini badala ya Vijijini hali ambayo Baadhi ya wananchi Kulalamika kuhusu hali hiyo.
Kwa Mujibu wa Mamlaka ya Maji Arusha Inaelezwa kuwa Mkoa wa Arusha una uhitaji wa Maji Lita Milioni 109 Huku mpaka sasa Mamlaka ya Maji Auwsa Inazalisha lita Milioni 200 zaidi ya kiwango kinacho hitajika huku tatizo kubwa likiwa ni Ubovu wa Miundo mbinu.
No comments:
Post a Comment