Mahakama ya Wilaya ya Dodoma leo Aprili 5, 2018 imepokea taarifa ya
vipimo vya kitabibu vya Tito Machibya (Nabii Tito) ili kujua kama ana
matatizo ya akili au la.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha
leo Alhamisi Aprili 5, 2018 amesema amepokea taarifa ya kitabibu kuhusu
Nabii Tito kutoka Isanga hivyo ataipitia ili aje atoe maamuzi siku ya
April 13 mwaka huu.
“Niseme tu kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa leo
asubuhi hivyo nitaipitia ili April 13, 2018 siku ya ijumaa niweze
kuitolea maamuzi,” amesema Karayemaha.
Nabii Tito ambaye hakuweza kuhudhuria kesi yake mara mbili mfululizo leo
amefika mahakamani baada ya hakimu Karayemaha kutoa maagizo ya
mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani au aletewe taarifa rasmi ya kwa
nini hafikishwi mahakamani kusikiliza kesi yake.
Februari, 2018 Nabii Tito alidai mahakamani kuwa yeye ana matatizo ya
akili yaliyosababisha kutaka kujiua na hivyo Mahakama kuamuru akafanyiwe
vipimo vya kitabibu ili kujua kama kweli mtuhumiwa huyo ana matatizo ya
akili au la.
Nabii Tito amerudishwa rumande hadi Aprili 13 kesi yake itakapotolewa uamuzi.
VIPIMO YA NABII TITO VYATUA MAHAKAMANI......HATMA KUJULIKANA APRILI 13
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment