Mwimbaji wa nyimbo za injili hapa nchini Emmanuel Munguree atambulisha
albamu yake ya pili iitwayo unaweza Yesu Habari Maalumu fm.
Mungure ametambulisha rasmi albamu
hiyo katika kipindi kinacho sikika
Habari Maalum fm kila siku ya Juma mosi saa 05pm hadi 07pm kiitwacho Top ten
ambacho hujumuisha nyimbo kumi ambazo zinafanya vizuri hapa nchini.
Mungure
amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa
neema na kibali, akaweza kufanya kazi
kubwa katika albamu hii ya pili, ambapo aliweza kutoa albamu ya kwanza huko
nyuma.
Aidha amesema katika upande wa usambazaji amewaomba
watu ambao wapo tayari kusambaza albamu hiyo wanaweza kuwasiliana nae.
Pia
ameeleza kuna utofauti kati ya albamu
yake ya kwanza na ya pili kwani albamu yake ya pili Mungu aliachilia mlango wa
kazi yake kutoka baada ya kukaa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment