Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo, Bi. Phily Muhebi mkazi wa Kilosa
amesema kuwa mwanaye alijeruhiwa vibaya kwa kipigo kutoka kwa waalimu
hao Machi 19, mwaka huu kwa kosa aliloelezwa na wanafunzi wenzake kuwa
ni baada ya mwenzake mmoja kulalamika kwa walimu kuwa amempaka upupu.
Taarifa za kujeruhiwa kwa mtoto huyo zimefikishwa Polisi huku Mama huyu
akilalamikia vitisho alivyopewa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo licha ya
mwanaye kuumizwa vibaya na walimu wake.
Mama wa Mtoto huyo amesema kwa sasa anahangaikia matibabu ya mwanaye
huyo huku akihofia uwezo wake wa kumudu gharama za matibabu, ambapo
ameiomba Wizara ya Elimu kuingilia kati suala hilo sambamba na kuwezesha
upatikanaji wa haki dhidi ya unyama aliofanyiwa mwanaye.
Uchunguzi wa Afya mtoto huyo unaendelea, huku taasisi ya mifupa MOI
ikiiahidi kutoa tarifa kamili punde baada ya uchunguzi wa kina wa
kitabibu wanaoufanya utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment