Gari la askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) waliokuwa wametoka katika sherehe za miaka 54 ya
Muungano Dodoma, limepata ajali baada ya kuigonga gari aina ya Noah na
kusababisha vifo vya watu wawili leo Aprili 27,2018.
Waliofariki, ni waliokuwa kwenye Noah, akiwamo mtoto miezi tisa, Amina Hassan na dereva wa Noah, Zindao Cornell, askari wa JWTZ.
Kamanda wa Polisi, mkoa wa Morogoro,
Ulrich Matei amesema gari lililokuwa limebeba askari wa JWTZ, lilipata
hitilafu katika tairi na kuigonga Noah.
“Ni tatizo la kiufundi, kwa sababu gari
lililobeba wanajeshi lilipata hitilafu ya kukakamaa kwa tairi la mbele,
gari hilo likamvuta dereva upande wa kulia na likagonga Noah,” amesema.
Amesema askari sita wa JWTZ, walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Kadhalika ameongeza kuwa mama mwenye mtoto wa miezi tisa, amelazwa katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment