DODOMA
Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri majini na Nchi kavu (SUMATRA) kanda
ya kati Dodoma katika kupanga mji wake kuanzia kesho Alhamisi Machi 29 mwaka
huu, njia za daladala zitabadilika na kurefushwa ikiwa ni pamoja na
kufuta stendi ya Jamatin, badala yake magari hayo yatakuwa yakiishia NaneNane
stendi mpya ya Mabasi.
Akizungumza jana, Ofisa
Mfawidhi Kanda ya Kati wa Sumatra, Conrad Shiyo alisema
njia hizo ndefu zimepangwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Manispaa ya
Dodoma na Chama cha Wamiliki wa Daladala Dodoma (UWEDO).
Shiyo alisema katika
marekebisho hayo, daladala zinazofanya safari kati ya Udom na Veyula zitakuwa
zikitoka Udom zinapita kwa Waziri Mkuu, Posta, General Hospital, Independence,
Sango na kupita NBC na kwenda Veyula na wakati wa kurudi kutoka Veyula zitapita
Paradise, Nyerere, Posta hadi Udom.
Aidha daladala zitakazo
toka Nala zitapita Sango, Hospitali ya Mkoa, Posta hadi Benjamin Mkapa
Hospitali na kurudi kwa kupitia Posta, General Hospitali, Independence hadi
Nala.
Hata hivyo Ofisa huyo wa
Sumatra alisema pia kutakuwa na njia ya Veyula hadi Nanenane, daladala zikitoka
huko zitapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Nanenane na kurudi kupitia CBE,
Carnival, General, Independence, Sango, NBC na kurudi Veyula.
Aidha daladala za kutoka
Chang'ombe hadi Nanenane, hizo zitapita njia ya Paradise,
Nyerere, CBE hadi Nanenane zitapita CBE, Carnival, Genereal
Hospital, Independence, Sango na kurudi Chang’ombe.
Magari ya kutoka St Gema
hadi Swaswa au Nanenane, zitapita Paradise, Nyerere, CBE hadi Swaswa
na kutoka Nanenane zitapita CBE, Carnival, General, Independence, Sango, NBC
kurudi St Gema.
Kuhusu daladala za
Nkuhungu hizo zitapita vituo vya Sango, General, CBE hadi Nanenane na
kurudi kwa kupitia kituo cha CBE, Carnival, Independence, Sango hadi
Nkuhungu.
Daladala kutoka Mkonze
zitapita vituo vya Kikuyu, Majengo, General, CBE hadi Nanenane na wakati wa
kurudi zitapita vituo ni CBE, Carnival, General, Majengo, Kikuyu
hadi Mkonze.
Alisema pia kwa daladala
zinazotoka Swaswa, Uzunguni na Nanenane na kurudi huko kupitia vituo vya CBE,
Carnival, kisha njia ya uelekeo wa barabara ya sabasaba hadi D.Center (Makole)
kisha kutokea mbele ya CBE na kurudi yalikotokea.
Shiyo alisema mabadiliko
ya njia yanalenga kuboresha usafiri mjini, kwani zitatakiwa katika daladala si
kuegesha bali kushusha pungufu ya dakika saba na kuondoka, lakini akawataka
wananchi wasisubiri Jamatini bali kwenye vituo vilivyoanishwa.
Alisema katika
kuhakikisha magari yote daladala na magari makubwa yanahamia Nanenane, vyombo
vyote vitasimamiwa na kuhakikisha kwamba magari makubwa yanahama na daladala
zinaanza safari ya kwenda huko ili kuwapa huduma wananchi wanaotaka kusafiri
kati ya mji na nje ya mkoa.
No comments:
Post a Comment