Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul
Makunda amewataka wananchi, wanasiasa pamoja na wadau mbalimbali kuepuka kuwapa
ujauzito wanawake na baadae kuwatekeleza.
Mkuu wa Mkoa Makonda ameyasema hayo Jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wakazi wa huo, ambapo
amesema kutokana na baadhi ya watu kuwapa ujauzito wanawake na kuwatekeleza
imepelekea kuharibu ndoto zao ambazo wamezipanga kwenye maisha yao.
RC Makonda amesema wamebaini kuna
baadhi ya viongozi serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini wamekuwa wakiwapa
wanawake ujauzito na baadae kuwateketeza.
Halikadhalika RC Makonda amesema kuna
baadhi ya watu wamekuwa wakiwatishia wanawake ambao wamewapatia ujauzito ama
kuwazalisha ili waepuke kutoa taarifa ya kitendo ambacho wamefanyiwa.
Hata hivyo amewatahadharia baadhi ya
wanaume ambao wamekuwa wakiwapa mimba wanawake kuwa watakapo bainika kuwapa
wanawake ujauzito watawachululia hatua za kisheria ili kuweza kukomesha tatizo.
No comments:
Post a Comment