Mwanaume mmoja anatuhumiwa kumuua mkewe
kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu za mwili wake kisha na yeye
mwenyewe kujinyonga hadi kufa kwa kutumia waya wa umeme wilayani Magu
ambapo kitendo hicho ni kosa kisheria.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi
amesema huyo ametambulika kwa jina la John Ntemi (23) mkazi wa Kijiji
cha Mahaha ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe Casta Edward.
Kamanda Msangi amesema inadaiwa wawili
hao walikuwa wanaishi peke yao na kabla ya tukio hilo kutokea wanandoa
hao walikuwa wakiishi kwa amani na upendo bila ya mgogoro wa aina yeyote
kati yao.
Ameeleza kuwa ilipofikia Machi 26, 2018
majira ya saa 6:00 mchana mwenye nyumba waliyopanga alipita karibu na
maeneo ya nyumba yao ndipo alipoona damu chini ya mlango na kutoa
taarifa kwa majirani pamoja na Jeshi la Polisi.
Kamanda Msangi amesema polisi walipofika
katika eneo la tukio waliwkuta mwili wa mwanamke ukiwa mlangoni ndani
ya nyumba eneo la tukio likionesha miburuzo ya damu toka chumbani hadi
mlangoni huku mlango ukiwa umefungwa kwa kufuli.
Uchunguzi wa awali unaonesha mauaji hayo
yalitekelezwa usiku wa Machi 25, 2018 kutokana na kuwepo kwa mvua kubwa
katika kijiji hicho kiasi kwamba majirani wasingeweza kusikia
kilichokuwa kikiendelea ndani kwa wawili hao.
No comments:
Post a Comment