Mwandishi wa habari Ansbert Ngurumo
ameijibu Serikali huku akisisitiza kupata vitisho, ikiwamo kutishiwa
maisha kutokana na namna alivyowakosoa viongozi.
Majibu ya Ngurumo yametokana na maelezo ya Serikali kwamba madai ya mwandishi huyo si ya kweli na yamejaa usanii.
Ngurumo ambaye kwa sasa amepewa hifadhi
nchini Finland, amedai kwamba Serikali haina rekodi nzuri juu ya watu
wanaofuatiliwa na kutekwa ndiyo maana haijui hata Azory Gwanda na Ben
Saanane waliko.
Amehoji kama maelezo yake ni usanii
wanaotenda maovu ya kuteka na kutesa watu ndani ya nchi, inakuwaje
Serikali isijue ni akina nani?
Ngurumo amesema wasamaria ndiyo
waliomsaidia kutoroka na kuzijua mbinu za watu waliokuwa wakitaka
kumdhulu, hasa katika mikoa ya Mwanza, Kagera na Dar es Salaam ikiwamo
kuyatambua magari waliyokuwa wakiyatumia kumfuatilia.
Amesema mbali na kutoa taarifa kupitia
mtandao wa kijamii wa Twitter Oktoba 3, 2017, hakutaka tena kupiga
kelele na badala yake aliendelea kupambana kimyakimya, kujilinda na
kumulika wabaya wake akiwa mbali.
No comments:
Post a Comment