Mamlaka ya Usafiri wa Baharini imesitisha safari zote za vyombo vya baharini kutokana na hali mbaya ya hali ya hewa Zanzibar.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana jioni, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Abdallah Hussein Kombo amesema wenye vyombo vya baharini ikiwamo meli, boti za uvuvi, ngalawa na mashuwa na wananchi kutojihusisha na safari za baharini mpaka hali itakapokuwa shwari.
Akizungumza na Mwananchi leo Machi 16, 2018, Kombo amesema hata hivyo huenda wakaziruhusu wakati wowote kuanzia sasa kwani hali imeanza kuwa shwari.
“Hivyo mamlaka inawaomba radhi wananchi wote kwa usumbufu,”imesema taarifa hiyo.
Safari za vyombo vya bahari zasitishwa

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment